+255 (0) 754 224440, banana@banana.co.tz

Banana Investment Limited ni kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa vinywaji mbalimbali vilivyo na
kilevi na visivyo na kilevi vitokanavyo na zao la ndizi.
Kampuni hii ilianza shughuli zake mnamo mwaka 1993 na makao makuu yake yapo mkoa wa Arusha barabara ya Nelson Mandela.
Banana Investment Limited inakaribisha maombi ya kazi kwa nafasi ya udereva kwa wale wote wenye
vigezo vifuatavyo;

A .SIFA ZA MUOMBAJI

 • Muombaji anatakiwa kuwa na cheti cha kuhitimu kidato cha nne (CSE)
 • Leseni ya udereva daraja “C” ya uendeshaji na uelewa mzuri wa alama za barabarani
 • Uzoefu wa kuendesha magari makubwa (mfano: Fuso, Canter, Scania n.k) kwa muda
  usiopungua miaka miwili bila kusabisha ajali (suala hili litafuatiliwa katika kitengo cha
  usalama barabarani).
 • Cheti cha majarabio ya ufundi daraja la III pamoja na cheti cha udereva kutoka katika
  chuo chochote kilichosajiliwa.

B. MAJUKUMU YA KAZI

 • Kuendesha magari ya kampuni
 • Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote
 • Kufanya uchunguzi wa gari kabla ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo
 • Kufanya matengenezo madogo mdogo ya magari
 • Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote
 • Kutekeleza kazi nyingine yoyote itakayopangwa na kiongozi wa kazi

C. MASHARTI YA JUMLA KWA MUOMBAJI

 • Muombaji awe raia wa Tanzania
 • Muombaji awe na umri usiozidi miaka 35
 • Barua zote ziambatanishwe na nakala ya vyeti husika pamoja na maelezo binafsi (CV)
 • Barua zote ziwe na anuani za uhakika pamoja na namba za simu za kuaminika

Jinsi ya kuomba:

Barua zote za maombi zitumwe kupitia anuani ifuatayo au kuletwa kwa mkono;

MENEJA RASILIMALI WATU
BANANA INVESTMENT LIMITED
P.O. BOX 10123
ARUSHA
TANZANIA
Au kwa barua pepe: mtoka@banana.co.tz

Mwisho wa kutuma barua za maombi ni tarehe 21st May 2016

Download PDF file – JB – Dereva